Burudani

Bonge la dada :Sipendi kucheza hadharani lakini kazi inalipa”

DAR ES SALAAM:DANSAanayetikisa kupitia wimbo wa Mbosso Khan “Aviola”, Queen Fraison, amefunguka kuhusu kazi yake ya unenguaji ambayo kwa sasa ndiyo inampa kipato.

Akizungumza baada ya kuulizwa kama anaipenda au haipendi kazi yake hiyo, Fraison amesema hana budi kuendelea nayo kwani ndiyo imemuweka mjini.

“Sipendi kucheza hadharani au kujidhalilisha. Mimi nina familia na nina wazazi kama ninyi, lakini sina jinsi kwa sababu hii ni kazi inayolipa na siwezi kuiacha. Familia yangu pia wanalijua hilo,” amesema.

Fraison ameeleza kuwa wengi hawajui umaarufu alioupata umetokana na sanaa ya kucheza, na kwa sasa amekuwa akipata mialiko mbalimbali ya maonyesho kupitia kipaji chake hicho.

“Sipo kwenye mambo mengine au tabia tofauti. Nacheza, nafanya kazi, namaliza, maisha yanaendelea kwa kuwa nina familia na wazazi wanaonitazama,” ameongeza.

Amefafanua kwamba kazi yake inapaswa pia kupewa heshima sawa na sanaa nyingine, ikiwemo muziki, uigizaji, au hata kazi ya ualimu.

“Ifike kipindi mashabiki waheshimu kazi yetu. Ni kazi kama nyingine yoyote mtu anavyoimba, anavyoigiza au mwanamitindo anavyofanya kazi yake,” amesema Queen Fraison.

Kwa sasa Queen Fraison anatajwa miongoni mwa wacheza shoo wanaofanya vizuri na kuvutia mashabiki kutokana na umahiri wake jukwaani.

Related Articles

Back to top button