Boman Irani: Sikuwahi kupata upendo wa baba

MUMBAI: MUIGIZAJI mkongwe mwenye mchango mkubwa katika filamu huko Bollywood, Boman Irani, ameweka wazi maisha yake ya utotoni na changamoto alizopitia baada ya wazai wake kufariki dunia.
Katika mahojiano hayo mkongwe huyo amesimulia kuhusu maisha yake ya utotoni yenye changamoto na jinsi alivyojitengenezea kazi yenye mafanikio katika showbiz licha ya changamoto mbalimbali.
Ameeleza kwamba hakuwahi kupata fursa ya kupendwa na baba, kwani baba yake alifariki kabla ya kuzaliwa, na kuacha pengo la kudumu la kihisia maishani mwake.
Katika mazungumzo na Raj Shamani kwenye podikasti yake, muigizaji huyo alizungumza kuhusu kifo cha baba yake: “Nilikuwa na matatizo mengine nilikuwa mtoto mwenye wasiwasi wakati wote sikuweza kujiamini hata kidogo.
Boman Irani anasema hata alivyoigiza katika filamu ya ‘ZEE5 Detective Sherdilerdil’, licha ya kukamilisha kurekodi filamu hiyo lakini hakupewa nafasi ya kuonekana kokote hadi baada ya miaka kadhaa ndipo akaonekana kwenye ZEE5.
Mkongwe huyo ameigiza na mashaa kadhaa wakiweno Sumeet Vyas, Diana Penty, Banita Sandhu, Chunky Panday na Ratna Pathak Shah.