BMT, TFF na Blueberry kuwapeleka mashabiki

DAR ES SALAAM: BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Wakala wa Usafirishaji Blueberry Travels, wametangaza mpango maalum wa kuwasafirisha mashabiki watakaosafiri kwenda Morocco kuisapoti Taifa Stars kwenye michuano ya fainali za mataifa ya Afrika ‘AFCON 2025’ inayoanza Desemba 21, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Mkuu wa kitengo cha maendeleo ya Michezo kutoka BMT, Benson Chacha, amesema mchakato huu umeanzishwa kutokana na maombi mengi kutoka kwa mashabiki waliotaka kufahamu utaratibu wa kusafiri kwa pamoja.

“Sisi kama Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na TFF tumekuwa tukipokea barua na simu nyingi kutoka kwa mashabiki wakitaka kujua utaratibu wa safari,
“Tumefanya mchakato na kupata kampuni ya Blueberry Travels ambayo itarahisisha mashabiki wengi kwenda Morocco kuishangilia timu ya Taifa,” amesema Chacha.
Mpango huo unalenga kuwapa mashabiki huduma bora na usafiri wa uhakika ili kuhakikisha Taifa Stars inapewa sapoti kubwa ugenini.
Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo amezungumzia malengo ya Taifa Stars ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye hatua ya makundi na kuingia mtoano na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa Afrika.
“Lengo ni kushinda kuhakikisha tunabeba ubingwa lakini ili kufika huko kuna mchakato, tunataka tutoke kwenye makundi, tuingia hatua ya mtoano,”amesema



