Billie Eilish, Ariana Grande kushirikiana kimuziki

NEW YORK: WAIGIZAJI maarufu wa pop kutoka nchini Marekani, waliwashangaza waliohudhuria katika onyesho la filamu ya ‘Wicked’ katika ukumbi wa maonyesho wa Directors Guild of America huko Los Angeles.
Hitmaker huyo wa ‘Bad Guy’ mwenye miaka 23, alimhoji hitmaker mwenzake wa ‘We Can’t Be Friends’ mwenye miaka 31, kuhusu kufanya wimbo wa Pamoja.
Ariana:”Billie tunahitaji kuingia studio Pamoja tufanye jambo” na Bilie naye alijibu: “Ningependa kufanya hivyo.”
Billie amekuwa shabiki mkubwa wa Ariana tangu akiwa mtoto na alifichua mengi kwenye chaneli yake kibinafsi ya YouTube.
Alikumbuka: “Na bado ninatumia chaneli ya YouTube ambayo imekuwa chaneli yangu ya kibinafsi tangu nilipokuwa na umri wa miaka 11. Nilikuwa tu ndani ya gari nikimwambia mama yangu kwamba anaweza kupata mahojiano yako ya zamani.’
Ariana ameeleza kwa utani: “Nilikuwa nikikuita Ari nilipokuwa na kaka yangu lakini wakati wote kaka yangu aliniambia nisikuite Ari,kwa sababu sikujui!”




