Diamond azindua Wasafi Festival

MSANII wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ leo amezindua tamasha la Wasafi Festival ambapo kwa mujibu wa taarifa yake litafanyika katika mikoa 10.
Diamond Platnunz amesema kuwa tamasha hilo litaanza September 2, 2023 Mtwara
Akiungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ‘Diamond’ amesema wamepanga kuchukuwa wasanii tofauti ili kuleta ladha katika tamasha hilo.
“Tutatumia jukwaa hii la Wasafi Festival 2023 kwa mambo Makuu matatu kuwaburudisha, kuwaelimisha na kuwapa watu fursa.
” Kwenye kila Mkoa tutakaoenda tutahainisha fursa za kibiashara, fursa za uwekezaji tutakuwa tunatembea na wawekezaji ambao wengine wataajiri watu wengine watataka kuwekeza kwenye Mikoa husika ili tuu kesho na keshokutwa kama taasisi isiwe imetumia mkusanyinyo wa Watanzania katika kufanya vitu ambavyo havina tija”
Tamasha Hilo mara ya mwisho lilifanyika Mwaka 2019.