Mastaa

Bien aingia kwenye mbio za Ng’ombe

NAIROBI: MWIMBAJI maarufu wa Kenya, Bien Aimé Baraza, ametoa amefichua kiasi cha pesa ambacho mmliki wa ng’ombe na mshindi hupata baada ya kushinda pambano la mchezo huo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Mic Cheque, Bien alifichua kuwa amemwita ng’ombe wake jina la bendi maarufu ya Kenya, Sauti Sol. Hata hivyo, ng’ombe huyo hajashiriki mashindano yoyote.

Bien alieleza awali alikuwa na ng’ombe mwingine aliyeitwa Shisundi, jina ambalo linatokana na neno la Luhya linalomaanisha giza.

“Niko na ng’ombe wawili, mojawapo anaitwa Shisundi, ni ya rangi nyeusi, kwa Kiluhya giza ina maanisha Shisundi, na mwingine ni Sauti Sol,” alifichua Bien.

“Shisundi aliuzwa, lakini Sauti Sol ndiyo anashikilia nafasi na inaendelea na mafunzo.”

Kulingana na Bien, mbio za ng’ombe ni utamaduni wa kina katika Kaunti ya Kakamega, hasa maeneo kama Ikolomani na Khayega, ambapo mashindano hufanyika kila Jumamosi asubuhi.

Mashindano makubwa ya ligi ya Ng’ombe huwa yanafanyika katika masoko ya maeneo mbalimbali, yakivuta umati mkubwa na michezo mingi ya kubetia.

“Mahali pekee panapofanyika mbio za ng’ombe ni Ikolomani, Khayega, Kakamega County, kila Jumamosi asubuhi,” alieleza.

Alipoulizwa namna mshindi anavyotangazwa, Bien alieleza kuwa kuna viashiria kadhaa vinavyoamua na kiasi cha pesa kinacholipwa kwa mshindi.

“Kuna bets nyingi watu huzibeti, ng’ombe unaweza kupigwa, au kushinda kwa kukimbia kwa kasi, kuna odds kuhusu ni mara ngapi ng’ombe atakutana na ng’ombe mwingine,” alifichua.

Aidha, alifichua kuwa ng’ombe huandaliwa kwa mashindano na watoto wa kijiji, ambao wanajua jinsi ya kuwatia nguvu na kuwasaka kuwa mashindano makali.

Pia, Bien aliongeza kuwa kwa miaka mingi amekuwa akiifikiria njia ya kufanya mbio za ng’ombe kuwa za kisasa na za muundo rasmi, ikiwa na ligi rasmi ambayo mashabiki wanaweza kubetia kama wanavyobeti kwenye mechi za soka.

“Nimekuwa nikifikiria sana kuweka ligi ya mbio za ng’ombe ili watu waweze kubeti, kwa sababu kama unatazama AFC, unaweza pia kutazama mbio za ng’ombe na ukapata faida,” aliongeza

Related Articles

Back to top button