Burudani

Bayothegreat atua na tuzo ya kimataifa ya utalii

DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa Reggae na Dancehall, Bayothegreat, amewasili leo jijini Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini akiwa na tuzo aliyotwaa hivi karibuni katika tuzo za kimataifa za International Tourism Film Festival Africa (ITFFA).

Bayo alishinda tuzo hiyo kupitia kipengele cha “Tourism Destination” kwa wimbo wake uitwao “Tanzania Unforgettable”, kazi inayobeba ujumbe wa kutangaza vivutio vya utalii na uzuri wa Tanzania kupitia muziki.

Ushindi huu si heshima tu kwa Bayothegreat binafsi, bali pia ni fahari kwa taifa kwa namna sanaa ya muziki inavyoendelea kutumika kama daraja la kukuza utalii wa ndani na kuitangaza Tanzania kimataifa.

Kupitia mafanikio haya, Bayothegreat ameonesha namna ambavyo wasanii wana mchango mkubwa katika kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kupitia vipaji vyao.

Related Articles

Back to top button