Mastaa
Barnaba: Watu ndio kitu Cha msingi maishani

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Barnabas Elias, amesema kuwa watu ndio kitu cha msingi zaidi katika dunia ya sasa, akisisitiza umuhimu wa kuishi kwa upendo na amani na kila mtu.
Akizungumza na Spoti LEO, Barnaba amesema hajawahi kuwa na matatizo au matabaka na mtu yeyote, ikiwemo vyombo vya habari, kwa kuwa anaamini maisha ni mafupi na kila mtu anapaswa kuthamini wenzake.
“Naishi vizuri na kila mtu kwa sababu maisha ni haya haya, hayajirudii. Jinsi unavyoishi ndivyo unavyoishia,” amesema Barnabas.
Msanii huyo ambaye amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva aliongeza kuwa mafanikio yake yamechangiwa pia na ushirikiano mzuri anaoendelea kuupata kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki.