Tetesi

Barcelona kumsajili Gündoğan

NAHODHA wa Manchester City, İlkay Gündoğan atajiunga na Barcelona kwa uhamisho huru wakati mkataba wake utakapofikia tamati mwezi huu.

Gündoğan mwenye umri wa miaka 32 alipewa ofa ya mkataba mpya na City lakini anafikiriwa alijadiliana dili bora zaidi la miaka mitatu na mabingwa wa Hispania, Barca.

Kocha Mkuu wa City Pep Guardiola alikuwa na nia ya kumbakiza Gündoğan ambaye alikuwa muhimu kwa timu hiyo katika kutwaa mataji matatu msimu huu.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani amecheza michezo 51 akiwa City katika msimu wa 2022-23 akifunga magoli 11.

Kuondoka kwa Gündoğan kunafuatia City kufikia makubaliano na Chelsea ya dili lenye thamani ya pauni milioni 30 sawa na shilingi bilioni 89 kumsajili kiungo Mateo Kovačić wa Croatia.

Gündoğan ataacha alama katika klabu ya Manchester City kama vile David Silva, Yaya Toure na Vincent Kompany ambavyo bado wanakumbukwa.

Related Articles

Back to top button