KwinginekoLa Liga

Barça yamsajili kinda matata wa kibrazil

MABINGWA wa Hispania Barcelona imethibitisha kumsajili kinda anayelijua soka kutoka klabu ya Athletico Paranaense ya Brazil, Vitor Hugo Roque Ferreira anayejulikana kwa kifupi, Vitor Roque.

Foward huyo kinda alianza kucheza timu ya taifa ya Brazil ‘Seleção’ Machi mwaka huu na amekuwa akihushwa kuhamia vilabu kadhaa vikiwemo Arsenal, Tottenham, Chelsea na Bayern Munich.

Hata hivyo, siku zote nia ya Rogue mwenye umri wa miaka 18 ni kujiunga na Barça na ada ya Euro milioni 40 sawa na shilingi bilioni 102 imekubaliwa haraka.

Mapema mwezi huu Barcelona ilikaribia kuthibitisha usajili wake lakini sasa imesema: “Mchezaji huyu anatarajiwa kujiunga na klabu yetu msimu wa 2024/25 na atasaini mkataba wa hadi msimu wa 2030/31 ukiwa na kipengele cha kununuliwa cha Euro milioni 500”.

Hivi karibuni mkurugenzi mpya wa michezo wa Barça Deco alisema : “Ni wazi nimeridhika sana, Roque ni mchezaji mzuri. Sasa ni suala la muda na klabu itatangaza,” amesema Deco.

Rogue alianza kuichezea Brazil akiwa na umri mdogo zaidi akivunja rekodi ya Ronaldo de Lima kwa siku nane.

Hivi karibuni alikuwa mfungaji bora wa michuano ya ubingwa wa Amerika ya Kusini kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 akifunga magoli sita nchi yake ilipotwaa ubingwa huo.

Rogue atabaki Ligi Kuu Brazil ya Serie A msimu ujao kabla ya kuwasili Barcelona msimu wa 2024/25.

Related Articles

Back to top button