Tetesi

Barca yakomaa na Messi

BARCELONA inaendelea kukomaa kumrudisha Lionel Messi na wameanza kwa kurejesha uhusiano baina yao kama ulivyokuwa awali, “limekuwa jambo la msingi” amesema Joan Laporta, Rais wa Barcelona.

Rais huyo alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu uwezekano wa Messi kurejea klabuni hapo, Laporta alisema suala hilo lipo katika mipango yao na wangependa kuwa na mchezaji huyo msimu ujao wa 2023/2024.

“Wapi Messi atacheza, atajua mwenyewe Xavi ( Kocha wa Barcelona ) hilo sio suala kwani ni mchezaji bora wa dunia.” Amesema Laporta.

Alipoulizwa kuhusu tetesi za Messi kwenda Al-Hilal ya Saudia Arabia, rais huyo alishangaa na kusema kuwa Barcelona itaendea kuwa kubwa ulimwenguni.

“Dau la Al-Hilal? Barcelona ni Barcelona. Hii timu inaweza kushindana na timu yoyote huko Arabia. Wanafanya kazi kubwa ya uwekezaji ila Barca ni nyumbani kwa Messi.” Ameongeza rais huyo.

Laporta amesema wameanza mikakati ya msimu ujao mara baada ya kutwaa ubingwa wa La Liga jana na sasa wanajiandaa kumuongezea mkataba mpya kocha wao Xavi Hernandez.

Hakutakuwa na tatizo kuhusu kuongezewa mkataba, anaelewa hali halisi ya klabu yetu, anastahili kuwepo anaitambua klabu vizuri.” Aliongeza Laporta.

Aidha, Rais huyo amesema uongozi wa klabu utaangalia uwezekano na kuamua hatma ya mshambuliaji Ansu Fati kwakuwa Barca bado inamuhitaji kwa sasa.

“Anataka kufanikiwa akiwa na Barca, ni mchezaji mwenye ubora mkubwa tutaona kitakachoendelea, tunataka aendelee kuwa nasi.” Ameongeza Laporta.

Related Articles

Back to top button