Kwingineko

Baba wa Odunlade Adekola afariki dunia

NAIGERIA: MUIGIZAJI wa Nollywood Odunlade Adekola ametangaza kufariki kwa baba yake, Mchungaji N.A. Adekola.

Muigizaji huyo maarufu alifahamisha kifo cha baba yake kupitia chapisho alilochapisha kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumamosi leo Julai 26, 2025, ambapo amechapisha picha ya baba yake na kuandika, “Rest on my daddy.”

Ingawa chanzo cha kifo hicho hakukiweka wazi ila tangazo hilo tayari limeibua majonzi kwa wanaomfahamu na wasanii wenzake pamoja na mashabiki wao.

Wengi wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumuenzi, wakimtaja kuwa mtumishi wa Mungu aliyejitolea katika kusaidia watu huku wakidai kwamba ameacha urithi wa kudumu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button