Kwingineko

Azpilicueta kutimkia Atletico Madrid

MIAKA 11 ya enzi za nahodha wa Chelsea César Azpilicueta imefikia mwisho na anatarajiwa kujiunga na Atletico Madrid.

Beki huyo wa Kihispania mwenye umri wa miaka 33 ameshinda mataji kadhaa akiwa Stamford Bridge yakiwemo mawili ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Azpilicueta amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Chelsea.

Katika video iliyooneshwa na Chelsea Azpilicueta: “Ni vigumu kuelezea jinsi gani nahisi, kumekuwa na mambo mazuri. Chelsea ni nyumbani kwangu siku zote kutakuwa hivyo na nina tumaini naweza kurejea nikiwa na jukumu tofauti,” amesema Azpilicueta.

Azpilicueta alianza soka timu ya utotoni ya Osasuna na alitumikia Marseille ya Ufaransa kwa miaka miwili kabla ya kuhamia Chelsea kwa ada ya pauni milioni 6.5 sawa na shilingi bilioni 19.36 Agosti 2012.

Beki huyo wa kati amefunga magoli 17 katika michezo 508 katika klabu hiyo ya London Magharibi na alichukua unahodha mwaka 2019 kutoka kwa Gary Cahill.

Related Articles

Back to top button