Kwingineko

Kaka nyota aliyehofia kucheza EPL

MADRID, Hispania: RICARDO Izecson dos Santos Leite, maarufu kwa jina la Kaka ni mwanasoka wa Brazil aliyewika sana akicheza nafasi ya kiungo cha ushambuliaji, ambapo kabla ya kustaafu alikuwa klabu ya Orlando City, lakini pia timu ya Taifa ya Brazil.

Kaka anayechukuliwa na wengi kuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa wa kizazi chake, amepata kutajwa mara tatu miongoni mwa wachezaji bora wa kuunda kikosi cha watu 11 kutoka miongoni mwa Fifpro.

Wapo watajiuliza Fifpro ni nini – ni taasisi ya kimataifa yenye uwakilishi wa wachezaji 65,000 wa kulipwa na kutoka humo, wachezaji bora hutajwa kila mara. Huyu alikuwa maarufu kuwa miongoni mwa hao 100 lakini pia alitoboa kwa walio bora kabisa miongoni mwa nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa).

Mbrazil huyo anasema ilikuwa awe kwenye kikosi cha Manchester City kuanzia 2009 kwa sababu aliitwa na kutakiwa kujiunga, lakini anasema alidhani haingekuwa vyema. Iwe iwavyo, leo Kaka akitazama upepo, anasema mambo yangekuwa tofauti na habari kuwa nyingine kabisa kwake na klabu.

Mkataba uliandaliwa, mambo yakawekwa tayari na ilikuwa ni yeye kumwaga wino katika dili la uhamisho ambao ungegharimu pauni milioni 100, lakini akaminya na hakusonga mbele, akaenda kwingine. Kulikoni alikataa?

Anasema kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya mchakato wa majenzi makubwa ya kikosi cha City wakati huo.

Si kwamba mambo yalikuwa mbali na ukamilifu, kwani tayari Manchester City na klabu yake ya Milan walishakubaliana juu ya ada, ambapo ilikuwa apate nyongeza kubwa ya mshahara, lakini baada ya tafakuri ya kina, akaona huenda kuvuka maji huko kutoka Italia hadi England hakungemwacha salama

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button