Nyumbani

Azam FC yaomboleza kifo cha Odinga

DAR ES SALAAM: KLABU ya Azam FC imetoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, aliyefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kupitia ukurasa wao rasmi wa mitandao ya kijamii, Azam FC imekumbusha tukio la kihistoria mwaka 2015 wakati Raila, akiwa miongoni mwa wageni mashuhuri, alikabidhi Kombe la Kagame kwa nahodha wa timu hiyo, John Bocco, baada ya Azam kuifunga Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2–0 katika mchezo wa fainali.

“Tunakumbuka kwa heshima na upendo ule wakati wa kihistoria. Pumzika kwa amani Baba,” imeandika Azam FC katika ujumbe wake wa maombolezo.

Odinga alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa waliokuwa na mahusiano ya karibu na wadau wa michezo ukanda wa Afrika Mashariki, hasa soka, ambapo alijulikana kwa uwepo wake katika matukio makubwa ya michezo na hamasa aliyokuwa akiionesha kwa vijana.

Kifo chake kimeacha simanzi si tu nchini Kenya, bali pia miongoni mwa mashabiki wa soka wa Afrika Mashariki waliomkumbuka kama “Baba”, jina lililojikita kutokana na mchango wake katika jamii na siasa za ukanda huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button