Asmah Majed akemea maswali: “Msiniulize kwa nini natembea kwa miguu”

DAR ES SALAAM: MSANII wa vichekesho, Asmah Majed, ameweka wazi msimamo wake kwa mashabiki na wadau wa mitandao ya kijamii kuhusu maisha yake binafsi, hususani suala la kutembea kwa miguu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Asmah Majed amesema kuanzia sasa hataki kuulizwa au kushangazwa anapokutwa akitembea kwa miguu, akisisitiza kuwa ni jambo la kawaida kwake na halina uhusiano wowote na masuala ya usanii.
Msanii huyo ameongeza kuwa hajali sana mambo yanayohusishwa na hadhi au maisha ya kifahari yanayodhaniwa kuambatana na usanii, na kwamba popote atakapomuona mtu asitafsiri mwenendo wake kwa mtazamo wa kisanii.
“Kuanzia leo mambo ya kunikuta nipo sehemu natembea kwa miguu mnaanza kuniambia ‘ehe Asmah unakuja hadi huku unatembea kwa miguu?’ Mnataka nitembee kichwa cha usanii wenu huko huko,” amesema Asmah Majed.
Kauli hiyo imeibua mjadala mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wameunga mkono msimamo wake wakisema ni ishara ya unyenyekevu, huku wengine wakitafsiri ujumbe huo kama ukosoaji wa mtazamo wa jamii juu ya maisha ya wasanii.




