Ligi Kuu

Andy Boyeli ni mwendo wa kazi

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Andy Boyeli amesema sapoti aliyooneshwa na mashabiki wa klabu hiyo katika mchezo uliopita dhidi ya KMC ni kama deni kwake kufanya kazi ya ziada kuendelea kufunga mabao mengi.

Andy Boyeli alifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC uliochezwa juzi Dar es Salaam.

Boyeli alisema anajivunia sapoti kubwa anayopata kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo na kuahidi kuendelea kupambana kwenye mechi zijazo.

Boyeli, aliyesajiliwa msimu huu akitokea Sekhukhune United ya Afrika Kusini huo ndio mchezo wa kwanza Ligi Kuu akitupia mabao kuonesha mwanga kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Boyeli alisema sapoti ya mashabiki kumuunga mkono kumemjengea ari ya kuonesha thamani yake kama mshambuliaji wa kuaminika katika kikosi hicho.

“Ninajivunia sapota wetu, wananipa hamasa zaidi ya kuendelea kupambana na kufunga mabao zaidi. Ni kama deni kwangu kufanya kazi kwa bidii,” alisema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button