Amorim atachezesha ‘watoto’ Ligi Kuu

MANCHESTER, KOCHA wa mashetani wekundu Manchester united amesema atatumia zaidi kikosi cha timu ya vijana kukamilisha michezo iliyosalia ya ligi kuu ya England akielekeza nguvu zaidi kwenye michuano ya Europa League ambayo timu yake ipo katika hatua na nusu fainali.
Manchester United walitinga hatua ya Nusu Fainali ya Europa League baada ya mchezo wa kusisimua dhidi ya Lyon ya ufaransa uliopigwa katika dimba la Old Trafford na mashetani hao wekundu kufanikiwa kushinda mabao 5-4 na kuzima ndoto za Lyon kwa jumla ya mabao ya 7-6.
“Tunahitaji kuwekeza nguvu zaidi kwenye Europa League hivyo tutajilipua kwenye Premier League, tunahitaji kila kitu chetu huku nitachezesha ‘watoto’ kwenye ligi natumai mashabiki wetu wa thamani watalielewa hilo” – amesema Amorim
Manchester United ni wa 14 kwenye Ligi wakiwa na pointi 38 walizokusanya katika michezo 32 ya ligi hiyo iliyochezwa hadi hivi sasa. Na Amorim anaamini mwenendo huo mbovu huenda ukafutwa na kutwaa taji la Europa.