Filamu

Amitabh Bachchan ashangazwa na mashabiki kunyeshewa mvua

MUMBAI:MKONGWE katika filamu nchini India Amitabh Bachchan ametoa shukrani zake kwa mashabiki wake waliomtembelea Jumapili nje ya nyumba yake Mumbai, Jalsa, licha ya mvua kubwa kunyesha.

Akitumia blogu yake, Amitabh ameeleza kuwa aliwainamia watu hao na kuwaombea.

Amitabh pia alishiriki rundo la picha, kwani watu kadhaa walionekana wamesimama kwenye mvua nyumbani kwake.

Amitabh Bachchan amekuwa akikutana na mashabiki nje ya Jalsa kwa miaka mingi sasa.

Katika picha, Amitabh pia ametoa picha yake mwenyewe na nyumba yake ya Jalsa. Akiandika: “Mvua ilikuwa ya mawimbi lakini walisimama pale, hawakupanga bajeti. Sina jibu lolote kwa upendo huu, sina maneno.”

Amitabh amesema aliwataka warudi nyumbani baada ya kuona mvua kubwa lakini mashabiki wake hao waliendelea kusimama katika eneo hilo. “Kwa wale ambao neema ya Mungu inaweza kusimamishwa kwangu na Mungu asiwepo kwa ajili ya upendo wao” ameeleza Amitabh.

Related Articles

Back to top button