Tetesi

Al Ittihad yashusha mtambo wa mabao

 MSHAMBULIAJI wa Nigeria John Ebuka amekamilisha uhamisho wa kuhamia klabu ya Ligi Kuu ya Misri, Al Ittihad, DAILY POST inaripoti.

Ebuka alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo yenye maskani yake Alexandria.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alihamia Al Ittihad kutoka klabu nyingine ya Misri, Al Masry.

Fowadi huyo alifunga mara moja katika mechi 12 za ligi akiwa na Al Masry baada ya kuwasili kwa mkopo Januari.

Ebuka alifanya kazi na kocha mkuu wa Al Ittihad Ahmed Sami wakati alipokuwa Ceramica Cleopatra.
Anaungana na Mnigeria mwingine, Isaac Savior, katika Al Ittihad.

Al Ittihad itakuwa klabu yake ya tano ya Misri katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Related Articles

Back to top button