Afrika Ya Kaskazini

Al Ahly waacha malalamiko wakitwaa ubingwa wa 45

CAIRO:KLABU ya karne Al Ahly ya Egypt imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu nchini Misri hapo jana kwa mara ya 45 katika historia yake, baada ya kuwalaza Pharco mabao 6-0 katika mechi raundi ya nane kwenye hatua za mchujo (playoffs) kutafuta Bingwa wa Ligi hiyo.

Kwa matokeo ya mechi hiyo Al Ahly wanafikisha alama 58 kileleni mwa msimamo wa Ligi, na Wekundu hao wamefanikiwa kutwaa ubingwa bila kuzingatia matokeo ya mechi iliyokuwa inaendelea kati ya Pyramids na Ceramica Cleopatra, uliomalizika kwa Pyramids kushinda 5-1.

Tukio la kushangaza ni pale ambapo baada ya michezo hiyo timu zote mbili zilishangilia, Pyramids walisherehekea kama mabingwa wakibaki uwanjani na kusubiri Kombe la Ubingwa wa Ligi hiyo, wakati huo huo Kombe hilo lilikabidhiwa kwa Al Ahly katika uwanja wa Kimataifa wa Cairo.

Pyramids waliamini wanastahili ubingwa huo kwani Al Ahly walipaswa kukatwa alama tatu baada ya kutofika uwanjani kucheza mchezo wa Dabi ya Cairo dhidi ya Zamalek, lakini cha kushangaza FA ya Misri imewatunuku Mabingwa hao wa kihistoria Taji hilo.

Back to top button