Afrika Ya Kaskazini

Ittihad yaendelea kuwasaka wachezaji waliopotea

TANGIER, MOROCCO: Klabu ya Ittihad Tanger inaendelea na jitihada za kuwasaka wachezaji wake wawili ambao walitoweka katika Pwani ya Kaskazini mwa Morocco ya Mediterania Jumamosi iliyopita.

Wahudumu watano wa Ligi Kuu ya Morocco wanashiriki katika msako wa meli ya kifahari iliyokodishwa katika eneo la mapumziko la ufuo la M’diq, Kaskazini mwa jiji la Tetouan, ambayo wachezaji hao walikuwa wakisafiria.

Huduma za dharura ziliwaokoa watu watatu baada ya tukio hilo, lakini Abdellatif Akhrif, mwenye umri wa miaka 24, na Salman El-Harrak, mwenye umri wa miaka 18, bado hawajapatikana.

Oussama Aflah, Soumaimane Dahdouh, na Abdelhamid Maali, mchezaji wa kimataifa wa Morocco wa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20, waliondolewa baharini baada ya kuwa hatarini kwa masaa kadhaa.

Rais wa Ittihad Tanger, Mohamed Cherkaoui, alithibitisha kuwa “utafutaji wa wachezaji waliopotea bado unaendelea”. Pia, amewataka mabaharia na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii kuendelea kuwa macho na taarifa wanazosambaza kuhusu wachezaji hao.

Back to top button