Ahmed afunguka Simba kufungiwa

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amefunguka juu adhabu waliyokumbana nayo kutoka CAF akieleza kuwa ni muda wa kujifunza kutokana na makosa.
Katika ukurusa wake wa Instagram Ahmed ameeleza haya…
“Baada ya jana kupokea hukumu ya CAF kuhusu kufungiwa Mashabiki katika mchezo wetu dhidi Costantine kumekua na mawazo na maoni mengi.
Wapo wanaosema tiketi ziendelee kuuzwa ili Wana Simba tuchangie faini iliyotozwa klabu yetu
Wapo wanaosema klabu iandae utaratibu maalumu watu wachangie kuipunguzia klabu mzigo wa adhabu ya faini hiyo
Na wengi wamesisitiza iandaliwe sehemu maalumu Wana Simba tukutane tuangalie kwa pamoja mechi
Kwanza niseme nimefurahishwa na fikra za Wana Simba kulichukua hili kuwa tatizo letu sote na tuko tayari kulitatua kwa pamoja
Pili niwaombe Wana Simba tutulie wakati huu ambao Viongozi wetu wakiangalia namna sahihi ya kuliendea jambo hili
Tatu niwatoe hofu Wana Simba kuwa adhabu yetu inahusu mechi moja tuu ya Jumapili, Robo Fainali tutaendelea na utaratibu wetu kama kawaida wa kwenda Uwanjani
Nichukue nafasi hii kuwapa pole Wana Simba wote ambao tumeumizwa na kadhia hii iliyotokea kwa mara ya kwanza katika maisha yetu
Mwisho kabisa ili kuepuka kupata maumivu kama haya ya kukosa kuiona Live timu yetu ikicheza mchezo muhimu kama huu hatuna budi sisi Mashabiki kujifunza kupitia sakata ili lisijirudie tena”ameeleza habari.