Mahusiano

Aggy Baby atoa ushauri wa Valentine:

“Zawadi iendane na thamani yako”

DAR ES SALAAM:MREMBO na mwanamitindo maarufu, Aggy Baby, amewataka wanawake kuhakikisha wanapokea zawadi za Valentine zinazoendana na thamani yao halisi.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Aggy Baby amesisitiza kuwa siku ya wapendanao ni muhimu kuthaminiwa kwa vitendo vinavyoonesha upendo wa kweli.

“Hakikisha anakupa zawadi ya Valentine inayoendana na thamani yako. Akikupa maua, ujue thamani yako ni sawa na hayo maua yenyewe,” ameandika Aggy Baby.

Kauli hiyo imezua mjadala mtandaoni, huku baadhi ya watu wakimuunga mkono kwa kusisitiza umuhimu wa kuthaminiwa, na wengine wakitoa maoni tofauti kuhusu tafsiri ya zawadi na upendo katika mahusiano.

Valentine huadhimishwa kila mwaka Februari 14, ambapo wapenzi huoneshana mapenzi kwa kubadilishana zawadi mbalimbali.

Related Articles

Back to top button