Kwingineko

Ada za mawakala uhamisho kimataifa tril 2/-

ADA za mawakala kwa ajili ya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji wa soka mwaka 2023 zinakaribia pauni milioni 800 sawa na shilingi trilioni 2.4.

Kwa mujibu wa ripoti ya uhamisho wa kimataifa wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) baada ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho katika ligi kubwa zote barani ulaya, matumizi ya jumla katika mikataba ambako wachezaji wamehama nchi kati ya Juni 1 na Septemba 1, yalikuwa pauni bilioni 5.9 kwa soka la wanaume, ikiwa ni ongezeko la asilimia 47.2 ya mwaka uliopita.

Matumizi kwa soka la wanawake ni pauni milioni 2. 4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 140.8.

Katika ripoti hiyo, FIFA inathibitha kwamba jumla ya uhamisho 10, 125 umefanyika katika soka la wanaume dirisha la majira ya kiangazi, ongezeko la asilimia 2.2 huku matumizi yakiongezeka kwa zaidi ya asilimia 45.

Zaidi ya asilimia 75 ya uhamisho wa kimataifa ulihusisha angalau klabu moja ya Ulaya.

Katika klabu za Shirikisho la soka Asia(AFC), ambako Saudi Arabia ni sehemu yake, zimetumia pauni milioni 830, kiasi ambacho ni asilimia 14 ya matumizi yote ya uhamisho wa kimataifa.

Mbali na matumizi ya pauni bilioni 1.6 ya klabu za England, Saudi Arabia ina matumizi makubwa zaidi kuliko nchi nyingine yoyote, ikiwa na matumizi ya pauni milioni 701.6 katika klabu za nchi hiyo.

Related Articles

Back to top button