Abby Chams anakamua tu huko!

MSANII mahiri wa muziki, Abigail Chamungwana, maarufu kama Abby Chams, ameonesha mafanikio makubwa baada ya wimbo wake “Me Too” kupigwa kwenye Official UK Chart Show ya BBC1Xtra. Hili ni hatua muhimu katika safari yake ya muziki wa kimataifa.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Abby Chams ameonesha furaha yake, akitoa shukrani kwa BBC1Xtra na familia yake ya Sony Music kwa msaada wao mkubwa katika safari yake ya muziki.
Wimbo “Me Too” umetayarishwa na Bboy, mtayarishaji maarufu anayejulikana kwa kazi zake na msanii Harmonize, ambaye nyimbo zake zimekuwa na ushawishi mkubwa kwa mashabiki wa muziki Afrika Mashariki.
Ushirikiano huu umezaa matunda na kuthibitisha uwezo wao wa kuleta muziki wa kiwango cha juu.
Kwa sasa, “Me Too” inashika nafasi za juu kwenye chati mbalimbali za muziki Afrika Mashariki, jambo linalodhihirisha upokeaji mzuri wa wimbo huo na umaarufu wake unazidi kuongezeka.
Katika kusherehekea mafanikio haya, Abby Chams amemwalika Harmonize kwa Iftar kama ishara ya shukrani kwa msaada wake kwenye safari yake ya muziki.