Nyumbani

Kagoma amerudi, mtaweka wapi sura zenu?

DAR ES SALAAM: MENEJA wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ametupa dongo kwa wapinzani wao kuwa wataendelea kuteseka baada ya kiungo wao, Yusuph Kagoma kurejea uwanjani.

Kagoma alikosa mechi na Dodoma Jiji kutokana na jeraha alilopata katika mchezo dhidi ya Azam FC , Jumatano Oktoba 2, amerejea uwanjani kufanya mazoezi na wachezaji wenzake kujiandaa na mchezo wa kesho, oktoba 4 dhidi ya Coastal Union.

Ahmed Ally ameliambia Spotileo kuwa baada ya kukaa nje kwa muda wa siku saba, sasa Kagoma yupo fiti lakini kucheza mechi ya kesho ni mipango ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids.

Amesema kuumia kwa nyota huyo katika mchezo na Azam FC kulimlazimukukaa nje kwa ajili ya kutibu majeraha yake na sio kusimamishwa  na Kamati ya hadhi na haki za wachezaji.

“Mashine ya kuchanganyia zenge imerudi kazini , mtaweka wapi sura zenu, wale  mliosema kiungo wetu amesimamishwa kupisha kesi uchwara. Mungu akipenda Ijumaa (kesho) tutaendelea kupata raha za Kagoma,” amesema Ahmed.

Related Articles

Back to top button