Muziki

Ayra Starr, Tems ndiyo wasanii wa Nigeria wanaofuatiliwa zaidi kwa mwaka 2024

LAGOS: WAIMBAJI maarufu, Ayra Starr na Tems wametangazwa kuwa wasanii wa Nigeria wanaofuatiliwa zaidi kwenye mtandao wa huduma ya kuuzia muziki wa kidijitali Spotify kwa mwaka huu wa 2024.

Spotify ilitoa orodha ya nyimbo 30 bora zaidi za Nigeria zilifuatiliwa zaidi katika mtandao huo katika nusu ya kwanza ya 2024 na wasanii hao ndiyo wameonekana kufuatiliwa zaidi.

Katika nyimbo 30 Ayra Starr anaongoza katika wimbo wa ‘Santa’ alioshirikishwa na Rvssian pamoja na Rauw Alejandro wimbo ambao kwenye mtandao wa Youtube unawatazamaji 71.5milioni. Wimbo wa Ayra Starr ‘Commas’ ambao kwenye mtandao wa Youtube unawafuatiliaji 45.3milioni umeshika nafasi ya pili huku Terms akishika nafasi ya tatu na wimbo wake wa ‘Love Me Jeje’ wenye wafuasi milioni 6.9 katika mtandao wa Youtube.

Wimbo Mwingine wa Luciano na Omah Lay ulishika nafasi ya nne huku Burna Boy na Savage’s Metro ‘Booming Just Like Me’ wenye wafuasi milioni 1.6 wakishika nafasi ya tano.

Phiona Okumu ambaye ni Mkuu wa Spotify Kusini mwa Jangwa la Sahara, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Lagos alisema orodha hiyo ilitambua nyimbo za Wanigeria zilizosikilizwa zaidi kutoka nje ya nchi kati ya Januari 1 na Juni 30 2024.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button