
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja mkoani Mbeya.
Baada ya kuvutwa mkia katika mchezo uliopita dhidi ya KMC kwa sare ya mabao 2-2, Simba ni mgeni wa Prisons kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu kati ya Tanzania Prisons na Simba Juni 26, 2022 Prisons ilishinda bao 1-0.