Ligi KuuNyumbani

Simba yaiwinda Tanzania Prisons

KIKOSI cha Simba kinatarajia kuondoka jioni ya leo kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kuikabili Tanzania Prisons Septemba 14.

Akizungumza na Spotileo, meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu amesema leo asubuhi kikosi hicho kimefanya mazoezi ya mwisho Dar es Salaam.

“Maandalizi yetu yamekamilika na timu yetu itaondoka saa 12 jioni kuelekea Mbeya tayari kuikabili Prisons,” amesema Rweyemamu.

Amesema wachezaji wote wapo kambini akiwemo Joash Onyango ambaye alikosekana kwenye mechi kadhaa.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na upinzani kati ya timu hizo.

Katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu kati ya Tanzania Prisons na Simba Juni 26, 2022 Prisons ilishinda bao 1-0.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button