
NUSU fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank(CBFC) itakayofanyika tarehe 18 na 19 mwezi huu.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga itapambana na Ihefu katika nusu fainali ya pili kwenye uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha Mei 19.
Katika nusu fainali ya kwanza Mei 18, Azam itakumbana na Coastal Union kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.