Ligi Daraja La Kwanza
Enzo kufanyiwa upasuaji
BREAKING: KIUNGO wa Chelsea, Enzo Fernandez atakosa mechi zote zilizobakia za Ligi Kuu England, ambapo anatarajia kufanyiwa upasuaji wa hernia.
Muargentina huyo alitakiwa kufanyiwa upasuaji mwezi wiki kadhaa zilizopita ilishindikana kutokana na mchango wake kwenye timu hiyo licha ya maumivu aliyokuwa anayapata.
Enzo anatajiwa kuwa fiti kwenye kwenye michezo ya Copa America na mwanzoni mwa msimu wa EPL.
Kwa mantiki hiyo, kocha wa timu hiyo, Mauricio Pochettino huenda akawatumia Moise Caicedo na Conor Gallagher kwenye eneo la kiungo




