EPL

Pochettino atoa onyo la mwisho

MKUFUNZI wa Chelsea, Mauricio Pochettino amekasirishwa na mzozo wa nani angepiga penalti katika ushindi wao wa 6-0 dhidi ya Everton na amewaonya wachezaji wake kutorudia tena.

Nicolas Jackson na Noni Madueke walibishana kuhusu nani angepiga mkwaju wa penalti, kabla ya Cole Palmer kuchukua mpira na kufunga bao lake la nne.

“Siwezi kukubali aina hii ya tabia,” alisema Pochettino, niliwaambia ni mara ya mwisho sitaki kuona tabia ya aina hii,”amesema Pochettino.

Aliongeza: “Haiwezekani kuwa na aina hii ya tabia baada ya utendaji huu. Ikiwa tunataka kuwa timu kubwa, tunahitaji kubadilika na kufikiri kwa pamoja.”

Palmer alifunga penalti ya dakika ya 64 kwa The Blues mkwaju wake wa tisa wa penalti msimu huu.

Related Articles

Back to top button