Kalaba wa TP Mazembe afariki dunia

Ajali yakataisha uhai wa Kalaba wa TP MazembeNYOTA wa zamani wa Zambia na TP Mazembe, Rainford Kalaba amefariki dunia leo katika ajali ya gari nchini Zambia.
Kalaba, aliyezaliwa Agosti 14, 1986 amefariki akiwa na umri wa miaka 37, alilazwa hospitalini akiwa katika hali mbaya kabla ya kufariki dunia kutokana na majeraha ya ajali hiyo.
Taarifa za kulazwa hospitalini hapo awali zilitolewa na Frédéric Kitengie, Mkurugenzi wa Michezo na Meneja Mkuu wa TP Mazembe, ambaye alitaka watu kumuombea.
“Kweli kabisa! Rainford Kalaba hajanusurika katika ajali ya barabarani Jumamosi Aprili 13 nchini Zambia kati ya Kafwe na Lusaka », walitangaza TP Mazembe katika tamko kufuatia uthibitisho wa kifo chake.
Maisha ya Kalaba au TP Mazembe yalikuwa na mafanikio kadhaa, na kumfanya kuwa mmoja wa wanasoka wanaoheshimika zaidi katika eneo hilo.