Tottenham macho kwa Conor Gallagher
TETESI za usajili zinasema Tottenham inajiandaa kufanya mpango wa kumsajili kiungo wa England anayecheza Chelsea Conor Gallagher, 24, ambaye mkataba wake unafikia mwisho 2025. (Teamtalk)
Liverpool, Tottenham na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vilabu vyenye nia kumsajili beki wa England anayekiwasha Fulham ‘The Cottagers’, Tosin Adarabioyo, 26.
Hata hivyo, The Cottagers inataka kumpa ofa ya mkataba mpya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City.(Standard)
Tottenham pia inavutiwa na winga wa Barcelona na Brazil Raphinha, 27, ambaye hatma yake katika miamba hiyo ya La Liga haijulikani. (Sport – in Spanish)
Arsenal, Chelsea na Manchester United zinamwinda kiungo wa Ukraine wa klabu ya Shakhtar Donetsk Georgiy Sudakov,21, ambaye ana thamani ya pauni mil 85. (Teamtalk)
Bayern Munich inaweza kugeukia kwa Jose Mourinho, ambaye hana kibarua baada ya kutimuliwa Roma, ili achukue nafasi ya Thomas Tuchel anayeondoka iwapo itashindwa kumteua Xabi Alonso. (Mirror)
Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte pia anahitajika Bayern Munich. (La Repubblica – in Italian)




