Tetesi

Bayern yamfikiria Solskjaer kocha wa muda

TETESI za usajili zinasema Bayern München inamfikiria kocha wa zamani wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer awe mwalimu wa muda wa miamba hiyo ya Ujerumani iwapo Thomas Tuchel atafukuzwa. (Sky Germany)

Wakati huo huo Bayern München inatafakari kumteua kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso, ambaye amehusishwa kwenda Liverpool. (Athletic – subscription)

Manchester United inataka kumsajili fowadi wa Bayern München na Ufaransa Mathys Tel, 18,.(90min)

Chelsea inamfuatilia mshambuliaji wa Bologna na Uholanzi Joshua Zirkzee, 22, lakini inakabiliwa na ushindani toka Arsenal, Manchester United na Barcelona(Teamtalk)

Kiungo wa kijerumani Joshua Kimmich, 29, anatarajiwa kuondoka Bayern München mwisho wa msimu kutokana na kutoelewana na kocha Thomas Tuchel. (Bild – in German)

Aston Villa inafikiria kumsajili kiungo wa Red Bull Salzburg,19, raia wa Israel, Oscar Gloukh. (Football Insider)

Related Articles

Back to top button