Tanzanite kambini Feb 18

WACHEZAJI 23 wa timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) wataingia kambini Februari 18 kujiandaa na mashindano ya All African Games yatakayofanyika Ghana.
Wachezaji waliochaguliwa kuingia kambini chini ya kocha mkuu Bakari Shime ni magolikipa Husna Mtunda, Zulfa Makau na Mariam Shaban.
Mabeki ni Sarah Joel, Christer Behera, Vaileth Nicholas, Noela Luhala na Lydia Maximilian.
Viungo ni Koku Kipanga, Ester Maseke, Hasnath Ubamba, Jamila Rajabu, Winifrida Gerald, Aisha Mnunka, Joyce Lema, Jackline Shija, Alia Fikiri na Veronica Mapunda.
Washambuliaji ni Zainabu Mohammed, Neema Paul, Sabina Alex, Jamila Selestine na Asha Omar.
Mashindano ya All Africa Games yamepangwa kufanyika Accra, Ghana kuanzia Machi 8 hadi 23, 2024 Tanzanite ikiwa kundi A kwa wanawake.