World Cup

Wapinzani wa Stars Kombe la Dunia

TIMU ya Taifa ya soka (Taifa Stars) itaanza kampeni ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika 2026 Canada, Marekani na Mexico Novemba mwaka huu.

Taifa Stars ipo kundi E pamoja na Jamhuri ya Congo, Eritrea, Niger, Morocco na Zambia.

Itaanza kampeni hiyo ugenini katika mchezo wa kwanza dhidi ya Niger kabla ya kuikaribisha Morocco kati ya Novemba 13 na 21.

Stars itakuwa nyumbani kuivaa Eritrea kabla ya kupanda ndege kuifuata Zambia michezo itakayofanyika kati ya Juni 3 na 11, 2024.

Kati ya Machi 17 na 25, 2025 Stars itakuwa uwanja wa nyumbani kuikaribisha Jamhuri ya Congo kabla ya safari ya kuifuata Morocco.

Stars itakuwa ugegeni kukabiliana na Jamhuri ya Congo kabla ya kurejea nyumbani kuchuana na Niger kati ya Septemba 1 na 9, 2025.

Itamaliza michezo ya kundi E kwa mchezo wa ugegeni dhidi ya Eritrea baada ya mechi ya nyumbani dhidi ya Zambia kati ya Oktoba 6 na 14, 2025.

Related Articles

Back to top button