
BAADA ya kukipiga na Al-Hilal ya Sudan katika mchezo wa kirafiki huko Tunisia Azam sasa watashuka dimbani Jumatano hii kukipiga na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa pili wa kirafiki.
“Kesho kutwa Jumatano saa 1.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki tutacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Esperance, Mchezo huo utafanyika jijini Tunis kwenye uwanja utakaotajwa hivi karibuni.” Imeeleza taarifa ya Azam.
Mchezo huo ni wa pili baada ya kuwafunga Al-Hilalmabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa kirafiki.