Kwingineko
Twiga Stars kuivaa Crested Cranes leo

Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” leo inashuka dimbani katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kuikabili timu ya taifa ya wanawake Uganda “Crested Cranes’.
Mchezo huo utapigwa uwanja wa MTN Omondi uliopo Lugogo jijini Kampala, Uganda.
Twiga Stars itawakosa nyota 14 wakiwemo 12 waliopo kwenye timu ya Jeshi Tanzania katika mashindano ya dunia ya majeshi kwa wanawake huko Uholanzi.