Ligi KuuNyumbani

Lusajo kukiwasha Azam hadi 2025

BEKI wa klabu ya Azam, Lusajo Mwaikenda amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kutumika katika viunga vya Azam Complex.

Hadi sasa Azam imetangaza kusajili mchezaji mpya mmoja, Gibril Sillah raia wa Gambia huku ikiwaongezea mikataba wachezaji sita ambao ni Daniel Amoah, Nathaniel Chilambo, James Akaminko, Sospeter Bajanam, Abdallah Kheri na Lusajo Mwikenda.

“Beki mahiri kiraka, @sajoh_57, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kubakia kwenye klabu yetu. Mkataba huo unamfanya @sajoh_57 kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025,” imesema Azam.

Kabla ya mkataba huo mpya Lusajo aliongezewa mkataba wa miaka mitatu Azam Machi 2020.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button