Michezo MingineRiadha

Majaliwa ataka vipaji riadha viibuliwe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kuibuliwa vipaji zaidi vya wanariadha ili kuiweka Tanzania katika ramani ya mchezo huo.

Mwanariadha, Gabriel Geay.

Waziri Mkuu amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha bunge la bajeti akiwapongeza Gabriel Geay na Alphonce Simbu kuwa mfano wa kuigwa huku akiipongeza wizara ya michezo kwa kuendelea kuupa nguvu mchezo huo.

“Nitoe msisitizo kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na michezo kuibua wanariadha zaidi kuwatafutia fursa katika mashindano ya ndani na nje ili waendelea kunufaika na vipaji vyao,”amesema Majaliwa.

Mwanariadha, Alphonce Simbu.

Gabriel Geay aliibuka na medali ya fedha katika mbio za ndefu za Boston zilizofanyika nchini Marekani mapema mwaka huu, huku Alphonce Simbu akishinda medali ya shaba katika mbio za Osaka zilizofanyika Japan.

Related Articles

Back to top button