BurudaniFilamu

ZIFF: Ni zaidi ya kuonesha filamu

HEKAHEKA zinarejea katika mji wa utamaduni wa Stonetown, eneo la urithi wa dunia linalotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),
wakati Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) maarufu kama tamasha la majahazi linapoanza.

Tamasha la ZIFF ambalo ni tukio la filamu kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki na Kati, linalosimamia sinema barani Afrika na katika ulimwengu wa Bahari ya Hindi, hulenga
kuongeza ufahamu na kuangazia filamu kama sanaa, burudani na tasnia, na vivyo kupanua mawazo kuhusu haki za binadamu na uhuru.

“Tamasha si mahali tu, bali pia kuhusu miundo yake ya kibunifu na endelevu na mchango wake katika bustani yenye rangi nyingi ya sinema za dunia,” anasema Profesa Martin Mhando.

Filamu 86 zilizochaguliwa kwa ajili ya kuoneshwa katika tamasha ni dhahiri kuwa mitaa ya Mji Mkongwe itagubikwa na wapenzi wa sinema ambao watakuwa wanatoka kutoka jumba moja hadi jingine wakiangalia sinema, kutafakari na kujadili.

“Filamu zilizochaguliwa ni pamoja na filamu ndefu 18, filamu za makala 22 na filamu fupi 45 kwa ajili ya kushindanishwa kwa kuzingatia kwa ujumla kaulimbiu ya kujitambua. Katika filamu zilizochaguliwa Tanzania inawakilishwa na filamu 15,” anasema Profesa Mhando.

Katika tamasha hilo ambalo lilizinduliwa Dar es Salaam, Shindano la Sembene Ousmane Films for Development, linaloungwa mkono na The Deutsche Gesellschaft für Internationale Entwicklung (GIZ), litafanyika tena, likibainisha ukuaji mkubwa wa ubunifu katika filamu za Kiafrika.

Filamu kumi na sita zimeteuliwa kuwania shindano hilo, huku filamu tatu kila moja ikishinda Euro 3,000 ili kutoa filamu mpya kwa ajili ya ZIFF 2024. ZIFF ikiwa imepokea
zaidi ya filamu 2,700 kutoka pande mbalimbali za dunia, Afrika Mashariki ikipeleka filamu 206.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa ZIFF, Prof Mhando akizungumzia tamasha hilo la 26 linaloanza leo Juni 24 na kukamilika Julai 2 likiwa na mambo mbalim bali yaliyolenga kuwezesha utambuzi yaani kujitambua inataka kutafuta maadili ya mtu, kutambua imani ambazo ni za msingi kwa malezi na mageuzi ya mtu na
athari ya mambo mbalimbali ya ndani na nje kama vile jamii, familia, kabila, rangi,
utamaduni, eneo, fursa, vyombo vya habari, uwezo wa kujieleza na uzoefu wa maisha.

Tunapozungumzia hekaheka tunazungumzia filamu, mijadala, mabaraza, shughuli, matukio na mambo mengine ya kawaida yanayounda utambulisho ambayo yatakuwa yanafanyika maeneo anuai ya Mji Mkongwe.

Profesa Mhando akizungumzia utambulisho aliangazia ukumbsho wa safari yake moja aliyoifanya Dodoma alipotembelea Michoro ya Miamba ya Kolo iliyoko Kondoa ya Kati Tanzania.

Anasema wakati akiwa pale akitafakari wakati yupo eneo hilo aligundua kuwa
kipengele muhimu cha kuwepo kwa binadamu ni mawasiliano kwani miaka 30,000 iliyopita, ambapo ndipo inapokisiwa uchoraji wa Kolo umefanyika,wanadamu walipata mahali ambapo waliweza kufanya mawasiliano wakifafanua wao ni nani kupitia mawasiliano
ya aina hiyo.

Anasema ukiangalia mawasiliano hayo unaona miaka 30,000 iliyopita unaona haja ya
mawasiliano na kama Kolo, tamasha la ZIFF nalo linatoa utambulisho na kuweka  mawasiliano kupitia sanaa ambao ni msingi wa kufafanua na kutafuta utambulisho.

Programu ya tamasha inafanyika katika kumbi mbalimbali za kupendeza karibu na bahari ya Mji Mkongwe wa kihistoria, pamoja na Panorama ya Kijiji ambayo inaeneza tamasha kwa jamii za vijijini, Panorama ya wanawake, ambayo hutoa lengo kwa masuala ya wanawake na Panorama ya watoto ambayo hutoa kwa ushiriki wa watoto na vijana kuna filamu na majadiliano magumu yenye kutafuta usahihi wa makazi ya mwandamu katika akili na moyoni.

Kupitia filamu, ZIFF kwa mujibu wa Profesa Mhando inatazamia kila mara kupata sauti  mpya kwa nyota wanaotamba na wanaochipukia, huku timu ya kutengeneza programu ikitoa mtazamo mpana zaidi wa kazi muhimu zaidi za mwaka kutoka Afrika Mashariki na kutoka Nchi za Majahazi.

Kwa kuwa ni kituo kikuu cha kimataifa cha uoni wa filamu, utaona ukuu wa tamasha hili kwa kuangalia mwenendo wa filamu zilizoshinda katika ZIFF kwani zimekuwa zikivuta hisia za wasambazaji wakuu wa filamu yakiwemo majukwaa mbalimbali na kwenye safari za ndege.

Ikumbukwe kuwa Mshindi wa ZIFF 2021, Binti, Netflix na pia inatumika kama kiburudisho katika shirika la ndege la Qatar Airways. Mshindi wa ZIFF 2022, Vuta N’Kuvute, pia ipi kwenye Shirika la Ndege la Qatar na filamu ambayo ni uchaguzi wa ZIFF ya Mpiganaji pia ipo kwenye Shirika la Ndege la Qatar.

Unaweza kusema ni mafanikio haba lakini yapo mengine lukuki tangu tamasha limeanza  nalo ni kupaisha utalii na pia kuonekana dhahiri kwamba Zanzibar ni sehemu njema ya kuzalishia filamu.

Tamasha la ZIFF ambalo huadhimisha sanaa na tamaduni za Bara la Afrika, India, Pakistan, Ghuba, Iran na visiwa vya Bahari ya Hindi ni eneo la shindano la kimataifa la filamu, muziki
na katika kipindi hiki kisiwa kizima huwa ukumbi wa michezo na sanaa za maonesho, warsha, semina, makonga-mano na programu zingine zinazohusiana na sanaa na
kitamaduni.

Kitu kikubwa kikiwa ni filamu, programu yake inajumuisha maonesho ya filamu yenye ushindani na yasiyo ya ushindani, katika miundo tofauti ya makala na hadithi fupi za kubuni, dokumentari, vikaragosi na filamu fupi za Kiafrika ambazo huingizwa katika
shindano la kipekee la Sembene Ousmane ambalo hushughulikia maendeleo.

Ndani ya tamasha hilo kuna matukio makuu matatu yatatokea kutambuliwa kwa mataifa
yaliyoshiriki ukombozi wa Afrika Kusini kupitia sinema, shughuli itakayofanyika Alhamisi ijayo.

“Mataifa 8 yaliyounda kile kilichokuwa umoja wa kihistoria uliopelekea ukombozi wa Kusini mwa Afrika, (Angola, Botswana, Lesotho, Msumbiji, Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Nigeria) yatatambuliwa katika hafla ya kumbukumbu inayotokana na filamu zilizoibua sinema mpya. Harakati na misemo,” anasema Profesa Mhando.

Aidha, aliongeza kwamba mpango wa filamu na kumbukumbu huimarisha mshikamano kama mada inayobainisha ya maendeleo kutakuwa na majadiliano ya kuvutia mtengenezaji wa filamu na msomi Simon Bright na timu yake.

Aidha, kutakuwa na warsha kubwa ya kujenga uwezo itakayowahusu washindi wa ruzuku ya miradi ya utamaduni na sanaa bunifu.

Warsha hii itakayoambatana na maonesho inawajumuisha washiriki kutoka Afrika Mashariki na Ulaya. Ziff ni mmoja wa waliopata ruzuku pamoja na Sauti ya Busara, Nafasi Art Space, Muda Africa na CDEA zote za Tanzania.

Ukiachia mbwembwe za asubuhi na mchana jioni ya siku ya leo kutaoneshwa filamu ya ufunguzi, ya msanii nguli wa sinema Idris Sultan akiwa kwenye Married To Work. Filamu hii inaonesha Zanzibar kama kisiwa cha ndoto na mapenzi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button