Ligi KuuNyumbani

Ndoa ya Kakolanya na Simba yatamatika

KLABU ya Simba imetangaza kuachana na golikipa wake Beno Kakolanya.

Kakolanya ni mchezaji wa nne Simba kutangaza kuachana naye baada ya Mohamed Ouattara, Nelson Esor-Bulunwo Okwa na Victor Akpan.

“Uongozi wa klabu unaujulisha umma kuwa hatutaendelea kuwa na mlinda mlango, Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika,” imesema taarifa ya Simba.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Kakolanya ameandika: “Asante sana mashabiki kwa upendo wenu mkubwa Sana kwangu bila kusahau uongozi mzima wa @simbasctanzania.”

Timu mbalimbali ziko katika harakati za kuimarisha vikosi vyao kwa kuachana au kuandaa mikakati ya kusajili wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano.

Related Articles

Back to top button