Ligi KuuLigi Ya WanawakeNyumbani

Baobab Queens mikononi mwa Azam FC

KLABU ya Azam Fc imetangaza kuingia makubaliano ya ushirikiano na timu ya wanawake ya Baobab Queens ya  Dodoma .

Azam Fc wamefikia maamuzi hayo kutokana na kubanwa na kanuni mpya za shirikisho la soka barani Afrika ‘CAF’ ambazo zinazitaka klabu zote zitakazoshiriki michuano inayoratibiwa na shirikisho hilo kuhakikisha zinakuwa na timu ya wanawake au kushiriki katika uendeshwaji wa timu ya wanawake kuanzia msimu wa 2023/2024.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa Azam Fc imeeleza kuwa taratibu zote zimekamilika katika jambo hilo.

“Kwa makubaliano haya na Baobab, ni rasmi sasa klabu hiyo ya Dodoma itakuwa klabu dada ya Azam Fc kuanzia msimu ujao” ilieleza taarifa hiyo.

Related Articles

Back to top button