Fainali UCL: Taji muhimu kwa Man City

KLABU ya Manchester City leo inasaka taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya itakapokutana na Inter Milan katika fainali kwenye uwanja wa Ataturk Olympic katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.
Iwapo City itafanikiwa kutwaa kombe hilo itakuwa imekamilisha makombe matatu baada ya kunyakua Kombe la Ligi Kuu na FA England.
Kocha Mkuu wa City Pep Guardiola anafukuzia mafanikio ulaya kwa mara kwanza tangu alipotwaa Kombe hilo mwaka 2011 akiwa na Barcelona ambapo pia alitwaa mataji matatu miaka miwili kabla.
“Huu ni mwisho. Ligi ya Mabingwa ni mashindano ya kusisimua. Ni ndoto kabisa kutwaa taji hili,” amesema Guardiola.

Kocha Mkuu wa Inter Simone Inzaghi amesema ana imani ana kikosi kinachoweza kunyakua taji hilo.
“Ni mechi mihimu zaidi kwangu lakini naamani nina wachezaji wazuri kama Dzeko na Onana ambao wamecheza fainali kadhaa,” amesema Inzaghi.
Inter Milan ilitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya mwisho mwaka 2010.