Burudani

Nicki Minaj kuburuzwa mahakamani

RAPA wa Marekani, Nicki Minaj huenda akaburuzwa mahakamani kwa kushindwa kulipa baadhi ya vitu vya thamani kwa sonara. Wakili wake amesema hahusiki na anadai sonara huyo anamtumia kujitangaza tu.

Ilidaiwa kuwa Nicki alichukua vipande 66 vya vitu vya thamani ikiwemo seti ya pete kwa mkopo wakakubaliana muda maalumu kutoa pesa, alishindwa kufanya hivyo.

Imeelezwa Nick alirudisha vitu hivyo kwa madai ya kuwa ni feki hata hivyo baadhi vilikuwa vimeharibika kwa mujibu wa sonara.

Taarifa ya mtandao wa TMZ imesema kuwa mwanamitindo wa Nick Minaj, Brett Nelson alisaini mkataba na Roseark Jewelry wakakubaliana rapa huyo atakuwa anachukua baadhi ya vitu vya thamani kwa bili kwa ajili ya matamasha yake mbalimbali.

Hata hivyo, vyanzo vilivyo karibu na Nicki vinasisitiza kuwa kila kitu kilirudishwa kwa wakati kama ilivyoahidiwa na ni baada ya vitu kuwa mikononi mwa sonara huyo kwa muda ambapo duka hilo lililalamika kukosekana kwa jiwe.

Related Articles

Back to top button