AfricaAfrika Ya KaskaziniWorld Cup

Morocco yamtimua kocha miezi 3 kabla ya Kombe la Dunia

Kocha aliyesaidia Morocco kufuzu fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022 Vahid Halilhodžić ametimuliwa ikiwa ni karibu miezi mitatu kabla ya kuanza kwa fainali hizo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocoo limesema uamuzi wa kumfukuza kazi Halilhodžić umefikiwa kwa sababu ya tofauti zilizojitokeza katika kuiandaa timu ya taifa kwa ajili ya mashindano hayo.

Morocco imetaanza mchezo wake wa kwanza Novemba 23 dhidi ya Crotia iliyofika fainali za Kombe la Dunia 2018. Morocco pia itacheza na Ubelgiji na Canada katika kundi F.

Katika fainali za Kombe la Dunia 2014 Halilhodžić raia wa Bosnia aliiongoza Algeria kufikia 16 bora ambapo nchi hiyo iliondolewa katika muda wa nyongeza na Ujerumani iliyokwenda kuwa bingwa.

Related Articles

Back to top button