Kwingineko

Young kuondoka Villa

BEKI Ashley Young ataondoka Aston Villa kufuatia mkataba wake kumalizika majira haya ya joto baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili.

Mlinzi huyo wa kulia wa zamani wa England amecheza mechi 32 msimu huu ambao Villa imeshika nafasi ya saba Ligi Kuu(EPL) na kufuzu michuano ya Ligi ya Europa Conference.

Young mwenye umri wa miaka 37 alijiunga tena na Villa mwaka 2021 akitokea Inter Milan kwa mkataba wa awali wa mwaka mmoja kabla ya mkataba huo kuongezwa.

Alicheza klabu hiyo kutoka mwaka 2007 hadi 2011 kabla ya kujiunga na Manchester United akicheza michezo 250 katika misimu miwili.

Kabla ya kurejea Villa Park, Young alikuwa sehemu ya kikosi cha Inter kilichotwaa ubingwa wa Serie A katika msimu mmoja katika klabu hiyo ya Italia.

Mchezaji huyo pia alifurahia mafanikio kitaifa na kimataifa akiwa United akishinda taji la EPL, Europa League, Kombe la FA na EFL.

Related Articles

Back to top button