Nyumbani

Zimbwe, Kapombe mziki mnene

MABEKI wawili wa timu ya Simba, Mohamed Hussein ‘Zimbwe na Shomari Kapombe wamewaburuza mabeki wengine kwenye idadi ya mabao waliyotengeza msimu huu kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Zimbwe na Kapombe wote wametengeza mabao sita msimu huu wakiafuatiwa na Nicolas Gyan wa Singida Big Stars aliyepika mabao Matano, mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa amehusika kwenye mabao manne msimu huu huku Amos Kadikilo wa Geita Gold FC na Djuma Shabani wa Yanga wakiwa wametengeneza mabao matatu kila mmoja.

Kwa sasa kila timu imebakiza michezo miwili ili kulifunga rasmi pazia la ligi kuu kwa msimu huu.

Related Articles

Back to top button